Wachezaji wenzake na Jota kutoka Liverpool ambao wameonekana msibani hadi sasa huko Gondomar, Ureno ni pamoja na nahodha Virgil Van Dijk, Andrew Robertson, Alexis Mac Allister, Darwin Nunez, Curtis Jones, Federico Chiesa na Wataru Endo.


Aidha, wachezaji wa zamani wa Liverpool, Jordan Henderson na James Milner nao pia wameonekana sambamba na kocha mkuu wa timu hiyo, Arne Slot, huku nahodha wa Man United, Bruno Fernandes, nahodha wa Man City, Bernando Silva na straika wa Chelsea, Joao Felix nao wakijitokeza kutoa heshima zao za mwisho kwa Mreno huyo.





Mazishi hayo yatamuhusisha pia mdogo wa Jota aitwaye Andre Silva ambaye naye alifariki katika ajali hiyo.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement