TWIGA STARS YAONDOLEWA WAFCON, WABABE WAENDELEA KUSALIA MOROCCO
Katika mchezo huo, Twiga Stars ilitakiwa kupata matokeo ya ushindi tu ili iweze kuendelea kwenye hatua ya Robo Fainali ya mashindano hayo.
Kwa upande wa Ghana wamefanikiwa kufuzu hatua inayofuata huku Mabingwa watetezi Afrika Kusini nao ambao walimaliza kileleni mwa Kundi C baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Mali.
Ushindi wa Ghana, pamoja na kichapo kizito cha Mali, ulimaanisha Black Queens kumaliza nafasi ya pili kwenye jedwali kwa tofauti ya mabao na wenyeji Mali wakashuka hadi nafasi ya tatu.
Afrika Kusini inasalia Oujda ambapo itapambana na Senegal, mshindi wa tatu katika Kundi A, katika nafasi nane bora, huku Ghana ikikutana na Algeria mjini Berkane huku Mali ikimenyana na wenyeji Morocco katika mji mkuu Rabat.
Matokeo ya Jumatatu yaliifanya Botswana kuondolewa, huku Mares wakiweza kusonga mbele kama moja ya timu mbili zilizo katika nafasi ya tatu bora ikiwa mchezo wa Ghana na Tanzania ungemalizika kwa suluhu.