BAADA ya kuhusishwa na Trent Alexander Arnold, vigogo wa Real Madrid wamehamia kwa mchezaji mwingine wa Liverpool, kiungo Alexis Mac Allister na wote imepanga kuwasajili dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Licha ya ripoti kudai hawajawasilisha ofa yoyote kwa ajili ya wachezaji hao, inaelezwa ofa hizo wanaweza kuwasilisha baada ya msimu kumalizika,

Madrid inamtaka staa huyu ili iboreshe eneo lao la kiungo ambalo ndani ya misimu miwili ijayo linaweza kuondokewa na mastaa kama Luka Modric na Toni Kroos.

Kwa upande wa Trent wanataka kumchukua kwa ajili ya maboresho kwenye eneo lao la ulinzi na imekuwa ikivutiwa na kiwango alichoonyesha kwa muda mrefu.

Tangu kuanza kwa msimu huu Alexis amecheza mechi 45 za michuano yote na kutoa asisti saba, wakati Trent akicheza mechi 36 za michuano yote na kutoa asisti tisa.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement