MODRIC AMEAGA MADRID KATIMKIA AC MILAN
Modric ambaye ni mshindi wa Ballon d’Or mwaka 2018 akiwa ameshinda mataji 28 akiwa na Real Madrid yakiwemo mataji 6 ya klabu Bingwa Ulaya na mataji manne ya Laliga yangu atue klabuni hapo akitokea Tottenham Hotspur mnamo mwaka 2012 amesaini mkataba wa mwaka mmoja na AC Milan na chaguo la ongezeko la mwaka mmoja zaidi.
Mchezaji huyo raia wa Croatia anashikilia rekodi ya kuwa mchezaji wa Real Madrid aliyepambwa zaidi (mwenye vikombe vingi kuliko wote) kihistoria.
Ameifungia Real Madrid magoli 43 kwenye mechi 597 na mechi yake ya mwisho ni kipigo cha 4-0 dhidi ya PSG kwenye nusu fainali ya kombe la Dunia la Vilabu.