Kocha wa timu ya Taifa ya Ufaransa, Didier Deschamps ametaja kikosi cha wachezaji 25 kwa ajili ya michuano ya Euro 2024.

Kiungo wa zamani wa Chelsea, N’Golo Kanté amejumuishwa kikosini sambamba na nyota kadhaa wakiwemo beki wa Arsenal, William Saliba, kiungo wa PSG, Warren Zaire-Emery, mshambuliaji Olivier Giroud na Kylian Mbappé.

Winga wa Crystal Palace, Michael Olise, nyota wa Chelsea, Malo Gusto, Axel Disasi na Christopher Nkunku hawajaitwa.

Nyota wengine ambao hawajajumuishwa ni pamoja na Mohamed Simakan, Jean Clair Todibo, Ben Yedder, Mattéo Guendouzi, , Jean-Philippe Mateta, Jordan Veretout na Moussa Diaby.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement