ROBO FAINALI YA MASHINDANO YA WAZI YA TENISI LEO HAPATOSHI NCHINI ENGLAND
Kwa upande wa Wanawake, vita ya kukata na shoka inayosubiriwa kwa hamu ni kati ya washindi wa medali za Olimpiki, Mirra Andreeva ambaye anatarajiwa kuoneshana kazi na Belinda Bencic.
Lakini habari nyingine kubwa ya Wimbledon ni Robo Fainali upande wa Wanaume na huku utashuhudia mchezo mkali baina ya Mserbia, Djokovic dhidi ya Flavio Cobolli wa Italia, huku Muitaliano mwingine, Sinner yeye akiwa na kibarua kizito dhidi ya Ben Shelton wa Marekani.
Mchezo mingine wa Robo Fainali unaotabiriwa kuwa na ushindani mkubwa ni kati ya mshindi wa Medali ya Shaba ya Olimpiki raia wa Poland, Iga Swiatek dhidi ya Lidmila Samsonova, hii ikiwa ni mechi ya upande wa Wanawake.