PSG YATENGA TSH.247 BILIONI KUMSAJILI RODRYGO GOES
Taarifa zimedai kuwa klabu ya PSG ipo tayari kulipa kitita cha takribani Euro milioni 80 (Tsh. Bilioni 247), ikidhihirisha uhitaji wao mkubwa kwa mshambuliaji huyo mwenye uwezo wa kucheza nafasi tofauti katika safu ya mashambulizi.
Kwa sasa Rodrygo ana mkataba na Real Madrid hadi 2028 lakini, jina lake huenda likatikisa zaidi katika dirisha kubwa la usajili kuelekea msimu ujao.
Chanzo: Fichajes