MAKALA : KOCHA MPYA WA REAL MADRID ATAMBULISHWA RASMI
Nyota mchezaji mwenye ushindi wa taji la ligi ya mabingwa ulaya maarufu UEFA Champions League 2005 akiwa liverpool FC, katika fainal ilio maarufu dhidi ya AC Milan , ambapo liverpool walitoka nyuma kwa mabao 3-0 hadi kusawazisha 3-3 kisha kushinda kushinda kwa mikwaju ya penati, tuna muongelea Xabi Alonso alifunga bao la kusawazisha ,mechi hii inajulikana kama "maajabu ya Istanbul".
Alonso ambae pia awewahi kuwa mchezaji wa klabu ya soka ya Real Madrid ,ndio amerithi rasmi mikoba ya kocha wa zamani Madrid Carlo Ancelotti alio achia kazi, hivyo kocha wa Mpyaa Xabi Alonso amengia mkataba wakuitumikia klabu hio kwa miaka 4, 2025- 2028.
Real Madrid Club de Fútbol ni moja ya vilabu vikubwa na mashuhuri zaidi duniani, kilichoanzishwa tarehe 6 Machi 1902 jijini Madrid, Hispania. Klabu hii imekuwa maarufu kwa mafanikio yake ya kitaifa na kimataifa, na inajulikana kwa kuvaa jezi nyeupe – hivyo kupata jina la utani “Los Blancos” (Wazungu).
Mafanikio Makuu:
Ligi Kuu ya Hispania (La Liga): Zaidi ya mataji 35.
Kombe la Mfalme (Copa del Rey): Zaidi ya mara 20.
UEFA Champions League: Real Madrid ndio mabingwa wa kihistoria wa michuano hii, wakiwa wamechukua taji hili mara 15 hadi mwaka 2024 – zaidi ya klabu yoyote nyingine.
Kombe la Dunia la Klabu: Zaidi ya mara 5.
Nyakati Muhimu:
1950s: Enzi ya dhahabu iliyoongozwa na nyota kama Alfredo Di Stéfano na Ferenc Puskás, walipotwaa UEFA Champions League mara 5 mfululizo (1956–1960).
Galácticos Era (2000s): Klabu ilinunua nyota wakubwa kama Zinedine Zidane, Luís Figo, Ronaldo Nazário, na David Beckham.
2010s hadi sasa: Kipindi cha mafanikio chini ya kocha Zinedine Zidane, akiongoza timu kutwaa UEFA Champions League mara tatu mfululizo (2016, 2017, 2018).
Viongozi na Uchezaji:
Rais maarufu: Florentino Pérez (anayejulikana kwa sera ya kusajili nyota wakubwa).
Uwanja: Santiago Bernabéu, ulioko katikati ya jiji la Madrid, wenye uwezo wa kuchukua zaidi ya mashabiki 80,000.
Ungana nasi kupitia kisumbuzi @startimestz CH 161 (antena) CH 401 (Dish) pamoja na kwenye YouTube channel yetu ya #STBongoTV Kwa Taarifa zaidI