Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Burundi Intamba Murugamba Etienne Ndayiragije, ametaja kikosi kinachoratajia kuingia Kambini katika kujiandaa na mechi mbili za kutafuta kufuzu kombe la Dunia 2026.

Katika kikosi hicho amejumuishwa mchezaji Saidi Ntibazonkiza anayekipiga katika timu ya wekundu wa msimbazi Simba SC ya Tanzania huku pia golikipa wa klabu ya Namungo Nahimana Jonathan akiwa miongoni mwa walioitwa.


Burundi inatarajia kucheza michezo miwili ya kutafuta tiketi ya kufuzu kombe la Dunia, mchezo mmoja ukiwa umepangwa kupigwa nchini Malawi dhidi ya Kenya kwenye uwanja wa Bingu Juni 7,2024.

Baada ya mchezo huo Burundi itakwea pipa kuelekea nchini Morocco kwa ajili ya kupambana na Seychelles kipute ambacho kitaweza kupigwa katika uwanja wa Municipal de Berkane majira ya saa mbili usiku.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement