TWAHA KIDUKU ATAMBA KURUDI ULINGONI NA BALAA KIVINGINE
Ni baada ya takribani miezi nane kuwa njee ya ulingo wa masumbwi,super star huyo ametamba nakusema ameutumia muda huo barabara kuweza kujiandaa vyema kurejesha nguvu na kasi mpyaa ,pia kufanyia kazi ushauru na matamanio ya mashabiki ili kuendana na mahitaji ya soko la masumbwi kitaifa na kimataifa.
Tarehe 24 mwez Mei mwaka huu 2025 atakutana uso kwa uso na bondia machachari mwenye majina Limbani Lano kutoka nchini Malawi ,Kiduku ametamba nakusema pambano hilo ndilo pambano atakalo onyesha ubabe wake na utofauti katika mchezo wa ngumi ulingoni hivyo ataonesha muonekano mpyaa waina yake ya uchezaji sambamba na burudani ya kipekee tofauti na alivyo zoeleka huko mwanzo.
Twaha Kassimu Rubaha ni bondia mwenye rekodi ya mapambano 35, ushindi wa mapambano 24 (9 KO) huku akiwa amewahi kuchezea kichapo katika mapambano yake 10 (1 KO) , Aametoa sare moja tu bingwa huyu wa masumbwi.
Nimemuandaa bondia huyu hatari kucheza kiwango cha juu na kuonesha burudani ya aina yake , na akisisitiza kuwa maandalizi ya kumkabili uso kwa us bondia kutoka Malawi Lano yamesha kamilika na hivyo wata shuka milimani morogoro kwelekea jiji la Dar es salaam, siku moja kabla ya pambano yani tarehe 23 Mei 2025.