Michuwano ya pili kwa ukubwa barani africa ,imewakutanisha mara ya kwanza Simba na Berkane kwenye final ambayo imeanzia kuchezwa nchini morroco na kuja kuhitimishwa kwemye ardhi ya visiwa vya karafuu maarufu kwa jina Zanzibar, ambapo Berkane waibuka mabingwa kwa kuwa na magoli mawili ya nyumbani na goli moja walioshinda ugenini huku simba wakiwa wamepoteza kwa kufungwa magoli mawili ugenini na kushinda goli moja wakiwa nyumbani katika uwanja wa new  Amaan Complex uliopo mjini unguja.

                                   Kombe la Jipya la shirikisho

                                        Kombe la zamani la shirikisho


Dk Patruce Motsepe Raisi wa shirikisho la mpira wa miguu Africa ,ndie alio tambulisha na kulizindua kombe hilo jipya la shirikisho Africa ,bila kusahau pia alitambulisha pia hivi karibuni  kombe lile la ligi ya mabingwa barani africa ambalo linawaniwa na vigogo kutoka nchi ya South Africa  Mamelodi sundowns na Waarabu kutoka Misri Pyramids  ambao walichuwana na kutoka kiwanjani na sare ya bao 1-1 jijini Pretoria katika mechi ya kwanza ambapo mechi ya pili ya fainali kuchezwa siku ya Jumapili Tarehe 1 mwezi June 2025.


You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement