"Wakala wa John Obi Mikel alijaribu kunipa rushwa ya Euro 50,000 kabla ya michuano ya Olympics 2008,"
Amedai kocha wa zamani wa Nigeria, Samson Siasia.
Kocha huyo amefichua kuwa John Obi Mikel, ambaye alikataa kushiriki mechi za kufuzu kwa michuano ya Olympic mwaka 2008, alihitaji ajumuishwe kwenye kikosi cha mwisho baada ya timu hiyo kufuzu. Ili kufanikisha hilo, wakala wa mchezaji huyo alidaiwa kutoa kiasi cha Euro 50,000 kama hongo ili Mikel aitwe kwenye kikosi hicho, lakini kocha Siasia anadai alikataa pendekezo hilo la rushwa.