AZAM MSIMU HUU WA LIGI ULIKUWA FUNZO KWETU
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Azam FC Thabith Zakaria ameleza kuwa kwa msimu huu malengo yameendatofauti kutoka na kutofikia malengo katika mashindano mbalimbali ikiwemo Kombe la Shirikisho Barani Afrika.
“Matokeo ya timu kubwa hatujaridhika nayo, tulitaka kupata kikubwa zaidi ya hichi, angalau tungepata alama nyingi zaidi ya tulizopata msimu uliopita, kwenye mashindano ya Shirikisho Tanzania Bara tungepata zaidi ya msimu uliopita maana yake tunazungumzia Ubingwa hapo kwa sababu msimu uliopita tulikuwa Fainali na tukatolewa kwa Penati, maana yake ni ubingwa na tulitarajia hicho kitu lakini haijawezekana, imetupa hamasa ya kujiandaa vizuri msimu unaokuja, ” Thabith Zakaria “Zaka za kazi” – Mkuu wa KItengo cha Habari na Mawasiliano Azam FC.