SENEGAL KUCHUKUA NAFASI YA CONGO BRAZAVILLE CECAFA 4
Senegal inachukua nafasi ya Congo Brazavile ambayo imekwama kusafari kama ilivyokuwa imepangwa awali.
“Tunafuraha kutangaza kwamba Senegal imekubali kushiriki mashindano hayo baada ya Congo Brazaville kueleza kuwa wamekumbana na changamoto za vifaa na hawakuweza kufanya safari kama ilivyopangwa awali,” Amesema Auka Gecheo – Mkurugenzi Mtendaji CECAFA.
Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi Julai 21-27 kwenye Uwanja wa Black Rhino, Karatu Jijini Arusha