Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) limetangaza kuwa mashabiki 27,000 pekee ndio wataruhusiwa kuhudhuria mchezo wa michuano ya CHAN kati ya Kenya na Zambia utakaopigwa Jumapili katika Uwanja wa Kimataifa wa Michezo wa Moi, Kasarani.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ametoa wito kwa wanamichezo kushiriki mashindano ya Jumuiya ya Madola kama washindani wa kweli ambao wataonesha vipaji na kuiletea Tanzania heshima.