GOR MAHIA YATAJA VIGEZO VYA KOCHA WANAYEMTAKA
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Gor Mahia, kocha mpya ni lazima awe na Leseni ya CAF ‘A’ Pro au Leseni ya UEFA Pro, uzoefu wa kufundisha klabu au timu ya taifa ya daraja la juu kwa muda wa miaka nane sambamba na rekodi imara ya kushinda makombe ya ligi na mashindano makubwa ya kimataifa.
Kama hiyo haitoshi, kocha anayetakwia Gor Mahia ni lazima awe na sifa kama vile uongozi imara, ujuzi wa mawasiliano, utulivu katika presha kubwa na kukisimamia vyema kikosi chenye wachezaji walio na ubora wa hali ya juu na uwezo wa kimbinu.
Na muhimu zaidi, uzoefu wa soka la Afrika, uwezo wa kuzungumza lugha zaidi ya moja na uwezo wa kuendeleza vijana, pia ni vigezo vitakavyompatia kocha huyo nafasi ya moja kwa moja kuwa kocha wa Gor Mahia.
Zedekiah “Zico” Otieno ndio kocha aliopita kuifundisha club hio kocha huyo Aliacha nafasi ya kocha wa muda (interim) Gor Mahia mnamo Julai 2, 2025, mara tu baada ya kukosa mataji msimu 2024/25 – ligi na cup zote zikipotea kwa kutumia mabadiliko ya ndani klabuni